Tuesday, July 12, 2016

VIDEO: Mo Music kazungumza haya kuhusu uongozi wake uliopita….


Kama utakuwa unakumbuka Mo Music hivi karibuni aliingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutangaza kwamba ameachana na menejimenti yake iliyokuwa ikisimamia kazi zake.


Sasa Ayo TV imemtafuta na kumuuliza sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo na kusema…’Sidhani kama nitaliongea zaidi hilo kwanza ningependa kuwapongeza kwamba wamenitoa mbali mpaka hapa nilipofika, kitu ambacho sitaweza kuwasahau ni pale ambapo nilipokuwa nikipata matatizo wanaonesha ushirikiano mzuri sana’- Mo Music


CONFIRMED: Tarajia hii collabo ya Vanessa Mdee na msanii kutoka Nigeria


Baada ya kufanya collabo na KO wa South Africa, kituo cha Mtv Base kimeripoti collabo nyingine ya mrembo Vanessa Mdee  na hit maker wa mdundo wa My Woman Patoranking, mdundo ambao utatayarishwa na producer Dj Maphorisa, Mtu wangu usisahau kuniachia commentya ujio wa hii collabo hapa chini na wakali hawa wataziona hapa.

Henry kaacha kazi Arsenal kisa kocha Arsene Wenger


Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ambaye amestaafu soka na kuingia kwenye kazi ya ukocha katika klabu yake ya zamani ya Arsenal, Juy 12 2016 ameamua kutangaza maamuzi magumu kuhusu ajira yake ndani ya klabu ya Arsenal.

Henry ameamua kuacha kazi ya kuendelea kukifundisha kikosi cha vijana cha Arsenal, baada ya kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger kuamua kumwambia kuwa achague moja kama kufanya kazi ya ukocha ndani ya Arsenal au kuendelea na kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha Sky Sports.

Baada ya kauli ya Wenger imemfanya Thierry Henry ameamua kuacha kazi Arsenal na kuendelea na kazi yake ya uchambuzi, kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry aliwahi kuichezea Arsenal katika kipindi cha miaka zaidi ya 7 na baadae kwenda kucheza soka katika klabu ya New York Red Bulls ya Marekani.

Video: Berry Black – Kiganja

Msanii Berry Black kutoka visiwani Zanzibar. Ametoa video mpya ya wimbo unaitwa “Kiganja”, video imeongozwa na kampuni ya Kwetu Studio.

Video: Ge2 – Sitaki Tararira

Video mpya ya msanii wakike ambaye ni rapper Ge2 kutoka Mkubwa na Wanawe, wimbo unaitwa “Sitaki Tararira”. Video imeongozwa na Pablo. 

PICHA 6 : DC wa Korogwe alivyobeba tofali baada ya shule kubaki na darasa moja tu lililo salama

June 30 2016 ilikuwa siku  ya mwisho ambayo Rais Dk John Pombe Magufuli aliitoa kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kumaliza tatizo la madawati lililokuwa linasumbua kwa miaka mingi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukaa chini.

Baada ya baadhi ya mikoa kumaliza tatizo hilo kwa asilimia kubwa lipo pia tatizo la kuchakaa na upungufu wa madarasa jambo lililomfanya mkuu wa wilaya ya Korogwe Gabriel Robert kuingia mtaani kusaidiana na wananchi kujenga madarasa matatu kati ya saba ambayo yanahitajika katika shule ya msingi Makondora.

Kilichofanya Mkuu wa wilaya na wananchi kuingia site ni baada ya shule hiyo kubaki na darasa moja ambalo ni salama na mengine ni hatarishi kwa wanafunzi na kuta zinaweza kudondoka wakati wowote.


 Mkuu wa wilaya ya Korogwe Gabriel Robert


Kikundi cha kinamama LIMCA kiliposikia na kuona juhudi za DC kilijitokeza na kutoa mifuko 15 ya Cement. 





 

PICHA 20: Schweinsteiger wa Man United kafunga ndoa na staa wa tennis

Staa wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Man United ya England  Bastian Schweinsteiger leo July 12 2016 ametangaza kufunga ndoa na mpenzi wake raia wa Serbia Ana Ivanovic ambaye pia ni mwanamichezo.

Bastian Schweinsteiger amefunga ndoa na Ana Ivanovic ambaye ni mchezaji wa tennis ikiwa ni miaka miwili imepita toka mastaa hao wawe pamoja, Bastian Schweinsteiger na Ana Ivanovic wamefunga ndoa leo mbele ya ndugu jamaa na marafiki.



















 

Jay Z na Beyonce ni couple iliyoingiza fedha nyingi zaidi

Jay Z na mke wake Beyonce bado wataendelea kuwa mfalme na malkia kwenye muziki kwa muda mrefu.


Kwa mujibu wa Forbes, wawili hao ndio couple ya watu maarufu walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka jana kwa kuweka benki dola milioni 107.5.

Queen Bey peke yake aliingiza dola milioni 54 na kukamata nafasi ya 54 katika orodha ya mastaa 100 waliongiza fedha nyingi, huku mumewe akiingiza dola milioni 53.5 na kukamata nafasi ya 36.

Mwaka jana Taylor Swift na Calvin Harris walichukua nafasi hiyo.


Omarion na mpenzi wake Apryl Jones waachana

Staa wa muziki Marekani, Omarion na mpenzi wake Apryl Jones wameachana baada ya kufanikiwa kupata watoto wawili.


Omarion (31) na Apryl (29) wamefanikiwa kupata watoto wawili kwenye mahusiano yao ambao ni Megaa Omari na A’mei Kazuko mwenye miezi minne.

Kupitia akaunti ya instagram Omarion ameweka picha yenye ujumbe uliosomeka:



“your chiccckkkkkk!! . New everything! Stand by!! It’s a lot (feels) COMING YOUR WAY!! & If I don’t feel the music! You won’t either. Let’s make this a fair exchange. #Bodyonme #Reasons #lit#workedhardtochangemylife p.s. Tell your friends I’m playing different these days. . .,” ameandika Omarion kwenye mtandao huo.

Video: Mtoto wa Future ameanza kumuita mume wa Ciara ‘Baba’

Hivi karibuni Ciara alifunga ndoa na mchumba wake Russell Wilson nchini Uingereza. Na sasa mtoto aliyezaa na rapper Future ameanza kumuita Russell ‘Papa’ neno linalomaanisha ‘Baba.’ 


Video inayomuonesha mtoto huyo akimuita baba yake wa kufikia ‘Papa Russ’ imesambaa mtandaoni. Mtoto huyo anaonekana akimuomba busu Russell na yeye kumjibu ‘You’re so sweet.’

Hivi karibuni mahakama iliamua Ciara na Future wawe na haki sawa za kumleta mtoto wao aitwaye Future. 

Wilson na Ciara walifunga ndoa wiki iliyopita.

VideoMPYA: Diamond Platnumz na P Square wametuletea hii video yao mpya leo

Diamond Platnumz ambaye ni muda umepita toka athibitishe kufanya collabo na wasanii mapacha wanaounda kundi la P Square, Peter & Paul leo July 12 ameamua kuachia rasmi video hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki, video mpya Diamond ft P Square inaitwa ‘Kidogo’

VIDEO: Shilole azungumza hiki ili asiabike atakapokutana na Beyonce….


Perfect Crispin ni mtangazaji wa Clouds FM ambaye hapa anatusogezea stori zilizochukua headlines kutoka kwenye tasnia ya Bongo Fleva, ambapo leo July 12, 2016 ametusogezea hizi stori tatu ikiwemo ya Shilole kutafuta mwalimu wa kumfundisha lugha mbalimbali.

Ni kweli nataka nirudi darasani nisome lugha ya kingereza kwani ni lugha ambayo imekuwa ikinipa changamoto nyingi mno, kwa sasa ndo niko kwenye mchakato kwani unajua mwisho wa siku sitaki niaibike pale nitakapokutana na wakina Beyonce kwahiyo hii ni heshima kubwa kwenye muziki wetu wa Bongo Fleva’- Shilole


VIDEO: Shabiki wa Mbeya City aliyejaribu kutengeneza Helicopter


July 12 2016 headlines za teknolojia zimechukua nafasi, mtu wangu wa nguvu nimekutana na documentary fupi ya kutoka mbeyacityfc.com inayomuonesha shabiki wa Mbeya City Adam aliyejaribu kutengeneza helicopter ambayo kwa mujibu wa Mbeya City wanasema haijaruhusiwa kufanya majaribio ya kupaa kwa sasa.

Adam ni mbunifu na helicopter sio kitu chake cha kwanza ambacho amewahi kutengeneza, Adam ambaye amejaribu kutengeneza helicopter kwa kutumia injini ya gari yake aina ya Toyota Ipsum,  aliwahi kutengeneza Mobile garage, yaani ni garage inayotembea ikiwa na kila kitu, zaidi tazama hapa documentary ya Adam




VIDEO: Mambo ya kufahamu pale sarafu ya Afrika Mashariki itakapoanza kutumika


Mchakato wa kuanzisha umoja wa fedha unaolenga kuanzishwa kwa sarafu moja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulianza januari 2011 wakati majadiliano kati ya nchi wanachama wa jumuiya wa Afrika Mashariki kuandaa itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha yalipoanza rasmi.


Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Lusajo Mwankemwa ametuelezea vitu hivi ambavyo unatakiwa kuvifahamu pale tutakapoanza kutumia sarafu moja ya Afrika Mashariki. zipo faida itakayopata Tanzania kutokana na umoja wa fedha na hasa kuwepo kwa sarafu moja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni pamoja na……….


Kupunguza gharama za kufanya biashara katika Nchi wanachama na hivyo kuhamasisha ukuaji wa biashara baina ya nchi wanachama na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.


Kwa kuwa na sarafu moja, umoja wa fedha utaepusha athari za ubadilishaji wa fedha ndani ya jumuiya.


Kuwezesha nchi wanachama kuwa na kiwango kidogo na tulivu cha mfumuko wa bei (low and stable inflation).


Kuwezesha nchi wanachama kuwa na viwango vidogo vya riba vya kukopa (low interest rates). 


Kutumia sarafu moja kutaleta uwazi katika bei na hivyo kuongeza ushindani wa soko ndani ya Jumuiya.


 Unaweza kuangalia video hii hapa chini


FC Barcelona imemsajili staa mpya Nou Camp


Klabu ya FC Barcelona ya Hispania leo July 12 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine atakayejiunga na klabu yao kuanzia msimu wa 2016/2017, Barcelona kupitia tovuti yao wametangaza kumsajili Samuel Umtiti kutoka klabu ya Olympique Lyonnais.

FC Barcelona imemsajili Samuel Umtiti kwa mkataba wa miaka mitano, kwa dau la uhamisho wa euro milioni 20, Umtiti atajiunga na kikosi cha Luis Enrique na atakuwa akicheza nafasi ya beki wa kushoto au beki wa kati.



Umtiti ambaye katika mechi nyingine za Olympique Lyonnais alikuwa akicheza kama nahodha, amecheza jumla ya mechi 170 akiwa na klabu hiyo katika kipindi cha miaka mitano na amefunga jumla ya magoli matano, Umtiti ana umri wa miaka 22, mkataba wake na Barcelona utamuweka klabuni hapo hadi 2021.

PICHA 10: Kutoka Ikulu wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa wakurugenzi wateule

 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassim Majaliwa 
 

Rais John Pombe Magufuli  
 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan 
 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Luhende Pius ambaye  kumekuwa na taarifa potofu juu ya taaluma yake.  
 

Kamishna wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst.) Salome Kaganda
 




Azam Tv Kuonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara, kumwaga Sh 23 bilioni Ligi Kuu


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF leo July 12 2016 limetangaza good news kwa mashabiki wa soka ambao huenda huwa wanakosa muda wa kwenda uwanjani kuangalia mechi, TFF leo imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano na Azam TV kwa ajili ya kuendelea kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.

Mkataba huu wa Azam TV sasa klabu itakuwa inapewa milioni 126 kwa awamu tatu tofauti na awali ilivyokuwa milioni 100, awamu ya kwanza na pili zitatolewa milioni 42, halafu awamu ya mwisho klabu inayomaliza nafasi za juu zaidi inalipwa zaidi kuliko iliyopo nafasi ya chini, hii inatokana na TFF na Azam TV kuamua kuleta ushindani.

Hafla ya kuongeza udhamini huo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na katibu mkuu Selestine Mwesigwa huku kampuni ya Azam ikiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wake Tido Mhando

Kwa mujibu wa mtandao wa instagram wa Azam umetoa taarifa hii:


Azam Media Ltd yashinda Tenda ya Kuonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine tena, udhamini mnono na wa Kihistoria Bilioni 23

Mgonjwa afariki, inadaiwa alilala nje ya Hospitali usiku kucha bila huduma, kisa?


July 12 2016 Kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea hii hekaheka kutokea Tandale Hospitali Dar es salaam ambapo mgonjwa aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje usiku kucha, mashuhuda wanasema hospitali walipopewa taarifa hawakujali.

Mashuhuda wanadai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye HekaHeka ya leo.
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa……….>>>’kaja toka jana kaingia ndani baada ya kuingia ndani kwa kuwa alikuwa hajiwezi alivyotoka akafikia akakaa hapa, basi alipofikia akalala mpaka leo asubuhi, tukawa waoga, tukaenda kituo cha polisi tukatoa taarifa, akaja polisi akamwangalia nae akaondoka, mwenyekiti akarudi tena nae akaondoka, mpaka inafikika saa 6;30 akawa anang’ata ulimi anakufa’

Kuisikiliza full story, bonyeza link hapa chini