Tuesday, July 12, 2016

Taylor Swift aongoza orodha ya mastaa walioingiza fedha nyingi 2016

Pesa inamliwaza Taylor Swift kutoka kwenye maumivu ya mapenzi.


Malkia huyo wa muziki wa Pop nchini Marekani, Taylor Swift ameongoza kwenye orodha ya jarida la Forbes kuwa mtu maarufu aliyeingiza mkwanja mwingi zaidi mwaka 2016 (The World’s Top-Earning Celebrity) akikadiriwa kuingiza zaidi ya $170 milioni.

Aliyekuwa mpenzi wake, Calvin Harris anashika nafasi ya 21 akiwa ameingiza kiasi cha $63 milioni. Floyd Mayweather ndiye aliyeongoza orodha hiyo kwa mwaka 2015 baada ya kuingiza kiasi cha dola milioni 300.

Hii ni Top 10 ya mastaa walioingiza fedha nyingi mwaka 2016.
2. One Direction $110 million
3. James Patterson $93 million
4. Dr. Phil McGraw $88 million
4. Cristiano Ronaldo $88 million
6. Kevin Hart $87.5 million
7. Howard Stern $85 million
8. Lionel Messi $81.5 million
9. Adele $80.5 million
10. Rush Limbaugh $79 million

No comments:

Post a Comment