Collabo ya Joh Makini na Davido, ilisharekodiwa, kupitia hatua zote za
kumalisha ngoma na sasa ipo tu kabatini ikisubiria muda muafaka, itoke.
Hiyo ni kwa mujibu wa Joh Makini mwenyewe alipokuwa akiongea na
mtangazaji wa Jembe FM, JJ. Amedai kuwa anachosubiria sasa ni kuangalia
namna ya kufanya video yake na kuitoa.
Pia ameshafanya collabo na muimbaji wa Nigeria Chidnima na video
ilishafanyika, alimshirikisha rapper wa Afrika Kusini, Khulichana pamoja
na wimbo mwingine aliofanya na rapper wa Ghana, EL.
No comments:
Post a Comment