Tuesday, July 12, 2016

Nisher atangaza kuirejesha tena Nisher Records

Anafahamika zaidi kama muongozaji wa video za muziki lakini Nisher ni mtayarishaji wa muziki pia, ukiongezea na vipaji vingine vingi alivyonavyo.


Staa huyo wa Arusha ametangaza kuirejesha tena studio yake ya muziki, Nisher Records. Ili kuwa na ujio wa kishindo, Nisher ametangaza ofa nzuri kwa wasanii wa kwanza kuingia ‘booth.’

Hata hivyo amesema kuwa kurejea tena kwenye utayarishaji muziki hakumaanishi kuwa ameachana na kuongoza video. Mwaka jana, producer huyo alitayarisha wimbo wa Fid Q, ‘Bendera ya Chuma’ aliyomshirikisha Ben Pol.

No comments:

Post a Comment