Mourinho ni miongoni mwa makocha wenye ‘mbwembwe’ nyingi sana duniani. Kupitia akaunti yake ya Instagram Mourinho ametania kwa kuandika, “if you want to visit the
country of the european champions visit PORTUGAL



Ureno ilifanikiwa kuifunga timu ya Ufaransa kwenye mchezo wa fainali goli 1-0 lililofungwa na Eder aliyeingia uwanjani dakika ya 79 akichukua nafasi ya Renato Sanchez na kufanikiwa kufunga goli dakika ya 109.
Hivi karibuni Mourinho ametangaza kuwa haoni sababu ya kukosa kila kikombe akianza kuifundisha timu ya Manchester United. Maneno hayo yametafsiriwa kama ni kejeli kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na Louis Van Gaal aliyekuwa kocha wa United.
No comments:
Post a Comment