Tuesday, July 12, 2016

Faiza Ally aeleza kwanini filamu yake ‘Baby Mama Drama’ imechelewa kuingia sokoni

Msanii wa filamu na Mama wa mtoto mmoja Faiza Ally amefunguka na kuzungumzia sababu ya kuchelewa kwa filamu yake mpya ‘Baby Mama Drama’.



Mwigizaji huyo ambaye haishiwi vituko, ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo imechelewa kutokana na kuwa na mlolongo mrefu wakati wa kuiingiza filamu hiyo sokoni.

“Baada ya kukamilisha filamu yangu, niliipeleka staps na stap wakaniambia sasa hivi hawachukui filamu ilimradi, wanachukua filamu ambazo pia zitaonyeshwa Sinema, kwa hiyo wanaangalia na viwango, na filamu yangu imechelewa kwa sababu ilikuwa na marekebisho kidogo,” alisema Faiza.

Mwigizaji huyo amesema mpaka sasa ratiba aliyonayo filamu hiyo itaingia sokoni mwezi wa tisa.Ndani ya filamu hiyo, Faiza ameigiza kama Mama huku Gabo Zigamba akichukua nafasi ya Baba.

No comments:

Post a Comment