Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amedai kuwa mtindo wa kuwapa
kipaumbele wasanii wachanga kuliko wakongwe kinawafanya wasanii hao
wachukuliwe poa.
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television
Jumatatu hii, Mr Blue amesema kitendo hicho kinawavunja moyo wasanii
wengi wakubwa hali ambayo inawafanya wasanii hao kukata tamaa.
“Sio tu wasanii wakubwa hawafanyi vizuri, lakini wanapewa heshima
inayostahili kwenye game?,” aliuliza Mr Blue. “Unakuta msanii ndogo ana
nyimbo mbili lakini analipwa pesa nyingi kuliko msanii mkongwe, vitu
kama hivi vinavunja moyo,”
Rapper huyo amewataka wadau mbalimbali wa muziki nchini kuwapa
heshima wasanii wakongwe kwani kufanyahivyo ni kuijenga tasnia ya
muziki.
No comments:
Post a Comment