Msanii wa muziki na mwalimu wa dance, Msami Giovani amesema kuwa haoni
kama kuna tatizo lolote endapo akiwa yupo kwenye mahusiano na staa wa
filamu Bongo, Kajala Masanja.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha E-News cha EATV, “Sioni kama kuna ubaya mimi kutoka na Kajala.”
“Sijasema nina mahusiano na Kajala ila ikitokea tukawa wapenzi
tunaweza kuzungumza mimi na yeye kujua hatima yake na mume wake ambaye
anatumikia kifungo kwa sasa,” ameongeza.
Masami na Kajala wamekuwa wakionekana wakiwa pamoja mara nyingi hali
ambayo imeibua maswali kwa mashabiki kuwa huenda wawili hao wakawa
wanatoka kimapenzi.
Hata hivyo hadi sasa ni Quick Rocka ndiye anajulikana kama mpenzi wa Kajala.
No comments:
Post a Comment