Baada ya baadhi ya mikoa kumaliza tatizo hilo kwa asilimia kubwa lipo pia tatizo la kuchakaa na upungufu wa madarasa jambo lililomfanya mkuu wa wilaya ya Korogwe Gabriel Robert kuingia mtaani kusaidiana na wananchi kujenga madarasa matatu kati ya saba ambayo yanahitajika katika shule ya msingi Makondora.
Kilichofanya Mkuu wa wilaya na wananchi kuingia site ni baada ya shule hiyo kubaki na darasa moja ambalo ni salama na mengine ni hatarishi kwa wanafunzi na kuta zinaweza kudondoka wakati wowote.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Gabriel Robert
Kikundi cha kinamama LIMCA kiliposikia na kuona juhudi za DC kilijitokeza na kutoa mifuko 15 ya Cement.
No comments:
Post a Comment