Thursday, August 18, 2016

Wema Sepetu na Petit Man wamaliza tofauti zao

Kwa miezi kadhaa sasa Wema Sepetu na Petit Man walikuwa wakichuniana hadi kuwafanya mashabiki waanze kuuliza maswali kupitia mitandao ya kijamii kutaka kujua kunani!
Lakini usiku wa August 16, wawili hao walionekana wakijirekodi video fupi na Wema akaiweka katika account yake ya SnapChat. Baadaye kulivyokucha Wema alionekana kupost video clip ile ile ya SnapChat kwenye Instagram kuandika hivi: Yes…! He has a piece of me… @officialpetitman_wakuachetz”
Kwa miaka mingi Petit alikuwa akifanya kazi na Wema kama msaidizi wake. Hivi karibuni aliongea na Bongo5 kuelezea tetesi hizo za kukosana na Wema.
“Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani,” alisema.

Idris Sultan aungana na Justin Bieber kufuta akaunti zao za Instagram

Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan ameifuta akaunti yake ya Instagram iliyokuwa na followers zaidi ya milioni 1.
Hivi karibuni kuliibuka tetesi za staa huyo kumwagana na mpenzi wake Wema Sepetu huku chanzo cha ugomvi huo ikitajwa ni kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake huyo kutompa support kwenye show zake.
Mashabiki wa Wema Sepetu wa mitandaoni maarufu kama ‘Team Wema’ waliibuka na kuanza kumtukana Idris hata hivyo staa huyo alivunja ukimya kwa kutoa yaliyokuwa moyoni kwenye mtandao wake wa instagram, aliandika:
“Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?.”
“Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja,” aliongeza.
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa.”
Hata hivyo Jumatatu ya wiki hii Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao akiwa Diamond.
Idris anaungana na staa mwingine wa Marekani, Justin Bieber ambaye mwanzoni mwa wiki hii na yeye aliifuta akaunti yake ya instagram iliyokuwa na followers zaidi ya milioni 77.


Perfect Combo ya Joh Makini kuanza kuchezwa MTV Base Alhamis hii

Video ya wimbo mpya wa Rapper Joh Makini, Perfect Combo aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Chidinma unatarajiwa kuchezwa kwa mara ya kwanza kwenye kituo cha runinga cha MTV Base kuanzia Alhamis hii, Agosti 18.
Video hiyo imeongozwa na Justin Campos aliyeongoza video yake ya ‘Nusu Nusu’ na ‘Don’t Bother’. Video hiyo inataoneshwa na kituo hicho kuanzia saa 12 jioni.
Tayari pia wimbo huo unaoneshwa Trace TV wiki nzima.

Utani wa Ellen DeGeneres kuhusu Usain Bolt watafsiriwa kama ubaguzi wa rangi

Kile kilichodhamiriwa kuwa ni utani kuhusu Usain Bolt, kimegeuka kuwa kitimoto kwa mtangazaji maarufu wa TV nchini Marekani, Ellen DeGeneres.
Jumatatu hii mtangazaji huyo wa talk show alitumia Twitter kuweka picha iliyotengenezwa na kumuonesha akiwa amebebwa mgongoni mwa mshindi huyo wa medali ya dhahabu raia wa Jamaica.
Picha hiyo ni ile ambayo sasa imekuwa maarufu sana mtandaoni ikimuonesha Bolt akichekelea ukingoni mwa mbio za mita 100 kwenye mashindano ya Olympics mjini Rio.
Maneno kwenye tweet hiyo yalisomeka: This is how I’m running errands from now on.”
Tofauti na matarajio ya Ellen, baadhi ya watumiaji wa Twitter waliitafsiri picha hiyo kama ishara ya kibaguzi kwa mzungu amebebwa mgongoni na mtu mweusi.
Lakini wengine walimtetea DeGeneres kuwa yeye na Bolt, aliyewahi kuhojiwa kwenye kipindi chake ni marafiki wakubwa. Mmoja aliandika: “If Usain was white, y’all wouldn’t care. We all know Ellen isn’t racist & didn’t mean any harm by that. Stop it.”
Ellen alijibu baadaye: I am highly aware of the racism that exists in our country. It is the furthest thing from who I am.”

Katiba inawatambua wabunge wote sawa – Dkt Tulia Ackson

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema hakuna Mbunge mwenye hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge.

Akizungumza hayo katika mahojiano maalumu katika kipindi cha DAKIKA 45, kinachorushwa na kituo cha ITV, Dkt Tulia alisema makundi yote ya wabunge yakishaapishwa wote ni wabunge wanaofanana katika hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa Bungeni.
“Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa,” alisema Dkt. Tulia
Aidha Naibu Spika huyo ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa.
“Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine aliweza kuelezea utendaji wake wa kazi tangu alipoanza kwa kusema, “nimeongoza Bunge bila upendeleo wowote ila nafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge na pia katiba inawatambua Wabunge wote wapo sawa.”

Shule za Kinondoni zajaza wanafunzi hewa kibao

Shule za msingi 68 pamoja na shule 22 za sekondari katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, zimebainika kuwa na wanafunzi hewa 5,996. Kati ya hao, wanafunzi 3,462 ni wanafunzi wa shule za msingi na 2,534 ni wanafunzi katika shule za sekondari.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi, ameitaja idadi hiyo jana katika ofisi yake wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya wanafunzi hewa waliopo katika wilaya yake.
“La kwanza tumemwagiza mkurugenzi kuwavua madaraka walimu wakuu 68 wa shule za msingi ambao watanyanga’nywa vyeo vyao kwa kosa la udanganyifu wa takwimu juu ya elimu bure,” alisema. “Lakini la pili tunaandikia tume ya utumishi wa walimu kupitia kwa mkurugenzi ambaye ndiyo muajiri wao kuhakikisha kwamba hatua nyingine kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya hawa walimu wakuu 68 wa wilaya ya Kinondoni, ambao wamedanganya katika taarifa zao na kuweka idadi ya wanafunzi hewa katika orodha ya wanafunzi wa elimu bure.”
Pia kwa upande wa walimu wakuu wa shule za Sekondari alisema, ” Walimu wakuu wa shule za sekondari wako chini ya katibu tawala wa mkoa, tumemuandikia katibu tawala wa mkoa kumuomba awavue vyeo vyao walimu wakuu 22 wa shule za sekondari zilizopo Kinondoni, ambapo wameleta takwimu za uongo na wameweka majina hewa ambapo zaidi ya milioni 60 zimekwisha kwenda kinyume na takwimu halisi katika shule zao.
Alielezea pia hatua zitakazochukuliwa dhidi wakuu hao, “Kwanza anashushwa cheo atakuwa mwalimu wa kawaida , lakini la pili atachukuliwa atachukulia hatua nyinginezo za kisheria kwa mujibu wa mamlaka ya utumishi wa walimu kwa shule za msingi na tatu atalipa fedha zote ambazo zimepelekwa kule kinyume na utaratibu kwa kutokana na udanganyifu alioufanya.”
“Hatutakuwa na huruma na mwalimu mkuu yeyote atakayefanya udanganyifu wa takwimu za elimu bure, tutamchukulia hatua kali za kisheria mwalimu yeyote ambaye ataghushi idadi ya takwimu za elimu bure kinyume na idadi halisi ya wanafunzi wa elimu bure.”

Video: Kid Ink feat. Jeremih & Spice – ‘Nasty'

Kid Ink celebrates with Jeremih and Spice in his latest video, a Caribbean-themed house party filled with gorgeous women dancing and vaping under black light.
“I like you when you nasty,” sings the Batgang boss, while Jeremih adds, “If she throw that ass, I’ma throw down some digits.”

Huyu ni mrembo wa SA aliyeonekana kwenye video za Diamond na Alikiba

Vita vya panzi ni furaha kwa kunguru. Mwanamitindo kutoka Afrika Kusini amebahatika kutokea kwenye video za wasanii heavyweight wa Bongo, Diamond na Alikiba.

Mrembo huyo ambaye anatumia jina la caelergangm kwenye mtandao wa Instagram, kwa mara ya kwanza amebahatika kuonekana kwenye video mpya iliyotoka hivi karibuni ya ‘Watora Mari’ ambayo Diamond ameshirikishwa na staa kutoka nchini Zimbabwe, Jah Prayzah.
“Amazing video ðŸ™‚ go check out the link in the bio of @jahprayzah Great working with you D,” ameandika mrembo huyo kwenye mtandao wake wa Instagram kwenye moja ya picha alizopiga na Diamond.
Siku chache zilizopita hitmaker wa ‘Aje’ aliweka kipande cha video kinachomuonyesha akiwa mwanamitindo huyo, Barakah da Prince na warembo wengine ndani ya nyumba moja huko Afrika Kusini ambapo kuna uwezekano mkubwa eneo hilo lilikuwa ni location.
Mrembo huyo anaweza akawa ndio video vixen wa wimbo huo mpya wa Alikiba ambao jina lake linadaiwa kuwa ni ‘ Kajiandae’. “@officialalikiba #kingkiba :),” ameandika mrembo huyo kwenye kipande cha video akiwa na Alikiba.


Mtoto wa kiume wa kinara wa madawa ya kulevya Mexico, El Chapo atekwa

Watu saba waliokuwa na silaha wamevamia kiota cha raha cha Puerto Vallarta kilichopo kwenye fukwe nchini Mexico na kumteka mtoto wa kiume wa mfanyabiashara maarufu wa madawa ya kulevya, El Chapo.
Kwa mujibu wa CNN, Jesus Alfredo Guzman, 29, mtoto wa – Joaquin “El Chapo” Guzman aliyepo jela, ametekwa pamoja na watu wengine sita Jumanne hii.
Utekwaji huo unakuwa pigo jipya kwa jitihada za Guzman akiwa jela kujaribu kuendeleza utemi wa cartel yake ya Sinaloa katika eneo hilo licha ya upinzani kutoka kwa kundi la Jalisco New Generation.
Jesus Alfredo na kaka yake Ivan Archivaldo Guzman wanasemekana kuendeleza shughuli za Sinaloa pamoja na mtoto wa El Capo aliyezaa na mwanamke mwingine, Ovidio Guzmán Lopez.
Jeshi la Mexico linaendesha msako wa kuwaokoa watu hao na kuwakamata wahusika. Jesus Alfredo ni mtoto mdogo kati ya watoto wawili wa El Chapo kwenye ndoa yake ya kwanza.
Kaka yake, Ivan Archivaldo Guzman, alifungwa Mexico mwaka 2005, lakini alitoka miaka miwili baadaye kutokana na kukosekana ushahidi.

Je, hili ndilo jina la ngoma mpya ya Alikiba?

Baada ya kuonjesha kile ambacho tutakiona kwenye video ya ngoma yake mpya, Alikiba anaweza akawa ametupa jina la wimbo huo.

Alikiba akiwa na warembo watakaoonekana kwenye video ya ngoma yake mpya
Mkali huyo wa Aje, ameanza kutumia neno #Kajiandae kwenye post zake mpya, huku kukiwa na uwezekano mkubwa kuwa likawa ndio jina la ngoma hiyo.
Hata hivyo bado haijulikani iwapo Kiba alienda Afrika Kusini kushoot video mbili au moja kwasababu hivi karibuni alidai kuwa alishoot video ya version ya Aje akiwa na rapper wa Nigeria, M.I.
Yeye pamoja na msanii mwenzake wa Rockstar4000, Barakah Da Prince walikuwa nchini humo kushoot video zao mpya.

Msafiri wa Kwetu Studios akanusha kusaini na Wanene Entertainment

Muongozaji wa video za Bongo anayefanya vizuri, Msafiri Shabani kutoka kampuni ya Kwetu Studio, amefafanua juu ya tetesi zilizoenea juu ya kusaini mkataba na kampuni ya Wanene kuchukua nafasi ya Hanscana.


Muongozaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hawezi kufanya kazi na kampuni ya Wanene kwa kuwa na yeye anamiliki kampuni yake.
“Hizo ni story tu sijafanya kazi na Wanene, sijawahi kufanya kazi na Wanene na sifanyi nao kazi kwa sababu mimi nina kampuni yangu inajitegemea,” amesema Msafiri.
“Sijasaini mkataba kwamba nafanya kazi na Wanene na wala Wanene hawajasaini na mimi,” ameongeza.
Msafiri ni mmoja kati ya waongozaji wenye uwezo mkubwa kwa sasa ndani ya Bongo ambao video anazotengeneza zinafanya vizuri kwenye TV tofauti tofauti.


Kumekucha: Serikali yatoa siku 7 kwa vyuo kurudisha fedha za mikopo zilizogawiwa kwa wanafunzi hewa

Wapo waliozitumia kujenga nyumba, wapo waliozitumia kununua vitu vya thamani na matumizi mengine, lakini sasa fedha hizo zitaanza kuwatokea puani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, ametoa muda wa siku 7 kwa wakuu wa vyuo na baadhi ya watendaji wa bodi ya mikopo kurudisha fedha zilizogawiwa kwa wanafunzi hewa.
Fedha hizo zimeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 3.
Akiongea na waandishi wa habari, Jumatano hii, Profesa Ndalichako alisema fedha hizo zimebainika kwenda kwa wanafunzi hewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na maafisa wa bodi ya mikopo wakishirikiana na taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa, TAKUKURU.
Vyuo zaidi ya 30 vilifanyiwa uhakiki huo ambapo ilibainika kuwa baadhi ya wanafunzi ambao walimaza chuo miaka mitatu iliyopita, bado wamekuwa wakiingiziwa fedha za mikopo kwenye akaunti zao.

FIFA yamfungia Rais wa zamani wa shirikisho la soka Afrika Kusini kwa miaka 6

Kamati ya maadili ya FIFA imempa kifungo cha walau miaka sita kwa aliyekuwa Rais wa shirikisho la soka la Afrika kusini, Kirsten Nematandani kwa madai ya kuhusika kwenye vurugu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyofanyika Afrika kusini mwaka 2010.
Miaka minne iliyopita alisimamishwa baada ya FIFA kupata ushaidi kuwa mechi ilipangwa na wabashiri washirika kutoka mashariki ya mbali.
Sambamba na hilo wachunguzi wa FIFA wamesema wamependekeza kifungo kirefu kwa aliyekuwa Rais wa wajumbe wa shirikisho la mpira wa Miguu la Zimbabwe, Jonathan Musavengana na kocha wa zamani wa Togo, Banna Tchanile, kwa madai ya kupokea hongo na rushwa.
Matokeo ya uchunguzi yatapitishwa kwenye jopo la majaji wa FIFA ili kufanya maamuzi.
Source: BBC

Mwandishi wa ‘Work’ ya Rihanna alitaka kumpa wimbo huo Alicia Keys

Mara nyingi muziki wa Marekani umekuwa ukiandikwa nyuma ya pazia na waandishi ambao wengi wao hawajulikani sana kwa watu kama wasanii wenyewe. Na wakati mwingine mwandishi huandika wimbo akimlenga msanii fulani lakini ukaja kuimbwa na msanii mwingine kabisa.
Na sasa mwandishi wa hit ya Rihanna na Drake, Work, PARTYNEXTDOOR amedai kuwa awali aliuandika wimbo huo kwa lengo la kumpa Rihanna, lakini label yake haikuupenda na hivyo alifikiria kumpa Alicia Keys.
“Label yake [Rihanna] haikuwa inajali kuhusu muziki wa Caribbean wakati huo,” aliliambia The New York Times na kuongeza kuwa kidogo aamue tu kukaa nayo kabla ya kufikiria kumpa Alicia Keys. Mwisho wa siku alisema Rihanna aliupigania.
PARTYNEXTDOOR anadai Rihanna alimwambia kuwa Work ni wimbo unaopendwa zaidi na familia yake.
Work ni wimbo uliofanywa vizuri kwenye chati duniani ikiwa ni pamoja na kukaa kwenye chati ya Billboard kwa muda mrefu.

Ni kosa kumwangalia mwanamke kwa sekunde 14 nchini India

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India.
Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani.
Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda.
Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake.
”Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”,alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi.
Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii.
Source:BBC

Bow Wow na Christina Aguilera waungana kwenye show mpya ya TV

Rapper kutoka Marekani, Shad Moss aka Bow Wow ataungana na Christina Aguilera kwenye kipindi kipya cha TV cha ‘Tracks’.
Kipindi hicho kinachotarajiwa kuanza kuonyeshwa kuanzia Septemba 1 mwaka huu na kitakuwa kinahusu watu tofauti kuweza kutaja majina ya nyimbo zinazochezwa kwa sekunde chache.
“It’s like a live concert where a game show breaks out,” amesema Bow Wow kwenye trailer ya kipande cha video ya show hiyo. Bow Wow anatarajiwa kuwa mtangazaji wa show hiyo huku Christina Aguilera akiwa mtayarishaji wake


Ajifungua mtoto kwenye ndege futi 30,000 angani

Mama mmoja anasherehekea kujifungua mtoto njiti bila kutarajia akiwa kwenye ndege futi 30,000 angani.

Mtoto huyo wa kike aliyepewa jina, Haven, alizaliwa salama baada ya labor kudumu kwa saa moja katika ndege ya Cebu Pacific iliyokuwa ikitoka Dubai kwenda, Manila Ufilipino.
Mama huyo, Missy Berberabe Umandal alishare picha kwenye Facebook na maelezo baada ya kujifungua.



Olimpiki: Kenya yashinda medali 4 za dhahabu

Mwanariadha wa Kenya Conseslus Kipruto ameishindia Kenya medali ya nne ya dhahabu katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Rio.

Mwanariadha wa Marekani Even Jager alikuwa wa pili na kujizolea medali ya fedha huku bingwa mara mbili wa michezo ya Olimpiki Ezekiel Kemboi akichukua nafasi ya tatu na kuishindia medali ya shaba Kenya.
Kenya imekuwa ikijishindia medali ya dhahabu katika mbio hiyo tangu mwaka 1994.Kenya imejishindi medali mbili za dhahabu siku ya Jumatano baada ya Faith Kipyegon kuibuka mshindi katika mbio za mita 1,500 upande wa wanawake.
Source: BBC