Rais Dkt John Magufuli ni mtu aliye busy na kazi nyingi za majukumu yake
lakini hupata muda wa kushika simu na kusoma kile kinachoandikwa kwenye
kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea Jumanne hii wakati wa kuapishwa kwa wakurugenzi wapya ikulu
jijini Dar es Salaam, alisema alikuwa akicheka tu alivyokuwa akisoma
comments za wananchi kuhusu uteuzi wake huo.
Anadai comments zilizomshangaza ni kuwa mmoja wa wakurugenzi hao ni
msomi wa cheti cha usimamizi wa hoteli wakati anajua aliyemteua ni msomi
wa shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara, MBA.
Aliwatania waandishi wa habari wampige picha mkurugenzi huyo aitwaye
Luhende aliyekuwepo kwenye hafla hiyo na yule wanayemdhania ni
mfanyakazi wa hoteli Sinza.
No comments:
Post a Comment