Monday, July 11, 2016

Zari na ndugu wa ukweni kwake haziivi, ujumbe huu wa Snapchat una majibu yote

Diamond Platnumz na Zari the Bosslady wapo kwenye mtihani mgumu unaozikumba familia nyingi za Kiafrika – maelewano hafifu na ndugu wa ukweni! 
Mama Tiffah yupo mjini alipokuja kumsalimia mchumba wake huyo na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mkwe wake. 

Licha ya Diamond kupost kipande cha video controversial Instagram wakiwa bafuni na mpenzi wake – wengi wanasema uso wa Zari unaonesha sura tofauti, ya huzuni tofauti na anavyoonekana mwenzie.


Kuna mengi yalitokea kwenye birthday ya Mama Diamond na ambayo yanazungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia urafiki usio wa kawaida wa dada yake Diamond, Esma na Hamisa Mobetto na mengine. Esma amelifafanua hilo kwa post ndefu Instagram.

 Lakini kubwa ni ujumbe wa kutatanisha wa Zari kwenye mtandao wa Snapchat unaoelezea jinsi ambavyo hajali ukoo mzima usipomkubali.


“Hakuna mtu mwenye uhusiano na dunia nzima, nchi au ukoo,” aliandika kwenye Snapchat, mtandao ambao wasanii wanaamini wana uhuru wa kufunguka zaidi.
“Huwa na uhusiano na mwanaume au mwanamke wao, ni mimi na yangu tu ndivyo vyenye maana. Unataka kujua kwanini? Ni sababu ilikuwa ni nyie wawili tu pindi mlipokutana. Na itakuwa ninyi wawili tu pindi mambo yakienda kombo kati yenu. Haitakuwa ukoo au nchi au mtu mwingine wa tatu,” aliongeza.
Bi. Sandra ambaye ni mtumiaji mzuri wa Instagramm aliweka petroli kwenye moto baada ya kupost picha ya Wema na Idris na kuwasifia: Uzalendo kwanza, umependeza sanaa mamy akee..”





Binamu wa Diamond, Romy Jones naye amepost picha kumpongeza shemeji yake wa zamani. Wanasema ushemeji haufagi lakini. 




Kuna mjadala mzito Instagram kuhusu issue hii. 
Tetesi za kuwa Zari hana maelewano mazuri na ndugu zake na Diamond zimekuwa zikiandikwa kwa muda mrefu na magazeti ya udaku. Kwa yaliyotokea, kuna asilimia nyingi za ukweli ndani yake.

Hakika Diamond kazi anayo!


New Video: Gnako Feat Nikki wa Pili – Laini

Rapper wa kundi la Weusi G Nako ameachia video mpya ya wimbo “Laini”, akiwa amemshirikisha Nikki wa Pili. Video imeongozwa na Freeman Richard.
 
 
 
 

New Video: Sultan King – Manyang’au

Msanii Sultani King kutoka Zanzibar, amechia video mpya ya wimbo unaitwa “Manyang’au”. Video imeongozwa na kampuni ya Kwetu Studio’s.

Video: Country Boy – AAh Wap

Rapper Country Boy ametoa video yake mpya ya wimbo wa ‘AAh Wapi‘, video hii imefanyika katika studio za Wanene ikiwa ndio video ya kwanza kutoka. Video imeongozwa na Khalfani Khalmandro.

Gadner asema mkataba mnono umemrudisha Clouds FM, azungumzia mahusiano yake na EFM

Mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G Habash, baada ya kurejea tena kwenye kituo chake cha awali, Clouds FM akitokea EFM, amefunguka na kuzungumzia maisha yake mapya ndani ya kituo hicho.


Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Gadner amesema kurudi Clouds FM sehemu ambayo alikaa kwa muda mrefu ni kitu ambacho kimemfariji sana.

“Maisha ni mazuri sana, ni maisha kama ukurasa mpya ambao nimeufungua,” alisema Gadner. “Namshukuru sana sana Mwenyezi Mungu amenipa kipaji lakini nawashukuru zaidi management ya Clouds FM kuona kwamba ninafaa nirudi pale tushirikiane tena, kwangu mimi naona ni kitu kikubwa japokuwa nilifanya kazi na Clouds FM kwa miaka 9 lakini bado hii nimeiona kama ni ukurasa mpya na nikitu kipya na ndio maana unasikia nasound kama mtu mpya,” alisema Gadner.

Pia mtangazaji huyo alizungumzia aliwezaje kurudi tena Clouds FM wakati tayari alishaanza maisha mapya na vituo vingine vya redio kama EFM.

“Ilikuwa ni vigumu sana kuondoka pale nilipokuwa (EFM) kwa sababu ya mazoea na urafiki ambao tulikuwa nao baina yangu mimi pamoja na staff ambao nilifanya nao kazi, baina yangu pamoja na viongozi, lakini wakati mwingine unapofanya uwamuzi, unahitaji kutumia hekima sana ili ufanye uwamuzi bila kuwa na hisia za kibinafsi, ufanye uwamuzi kutokana na nini biashara inataka, au ni nini maslahi yanataka na ndo utumie akili kuona kama maslahi yao. Zaidi ya hapo ujitahidi uondoke kwa mazingira yalio salama bila kukwazana na wale unaoachana nao, lakini ilikuwa ni ngumu, lakini kwa sababu Clouds FM walikuwa wananithamini kiukweli wamenipa offer ambayo ni kubwa sana na unajua wakati mwingine unamuomba mungu, lakini Mungu anakuletea bila kujua kama anakuletea nafikiri katika dua zangu ambazo nilimuomba Mungu aniongezee naona mkataba wangu mpya wa Clouds ameniongezea,”

Formation World Tour ya Beyonce yaingiza dola milioni 11 ndani ya siku 2

Ziara ya dunia, Formation ya Beyonce imeingiza dola milioni 11 katika siku mbili


May 27 na 28, muimbaji huyo alitumbuiza show mbili za live kwenye uwanja wa Soldier Field, Chicago. Baada ya kujaza siti 89,270, Queen Bey aliingiza $11,279,890 ndani ya siku mbili.

Kiasi cha fedha alizoingia kwenye show yake ya uwanja wa Wembley bado hazijatangazwa lakini aliuza tiketi zote.

Ziara yake itafikia tamati October 2, 2016.

VIDEO: Kauli ya Kamusoko baada ya kuwa nominated katika tuzo za VPL

Jumamosi ya July 9 2016 majina ya nominees watakaowania tuzo za Ligi Kuu soka Tanzania bara (VPL)  msimu wa 2015/2016 yalitajwa, July 17 2016 ndio siku rasmi ya utolewaji wa tuzo hizo, tuzo hizo kwa msimu wa 2015/2016 zitatolewa 13 kwa vipengele 13 vilivyotajwa.

Miongoni mwa majina au vipengele vilivyopo ni tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, ambapo katika Category hiyo ametajwa Thabani Kamusoko, Donald Ngoma wa Yanga ambao wote ni raia wa Zimbabwe na Vincent Agban wa Simba raia wa Ivory Coast. Ayo TV ilimpata katika exclusive Thabani Kamusoko, alitarajia kuwa nominated?

“Sikutarajia kwa namna nilivyokuwa nacheza naweza kusema sikuwa nimetarajia kuwa nominated katika TOP 3 ya wachezaji bora wa kigeni, lakini najisikia furaha maana kuwa nominated una kitu fulani ndio maana upo pale

muangalia hapa chini:VIDEO By AyOTv

VIDEO: Shabiki huyu mtoto wa Portugal akimbembeleza wa Ufaransa aliyekua analia baada ya kufungwa


Hakuna mtu ambaye hupenda timu anayoishabikia ifungwe au kushindwa kwenye fainali na katika hao mashabiki wako ambao wanahisia nzito zaidi kama huyu wa Ufaransa aliyeshikwa na machungu baada ya timu yake kushindwa kwenye fainali za EURO 2016 jana Ufaransa

WEMA NI BRAND: Bidhaa mpya ya Wema Sepetu… anavyoendelea kutengeneza pesa kwa jina lake

Nguvu ya mwigizaji staa wa Tanzania Wema Sepetu  kutengeneza zaidi bidhaa zenye jina lake na kuziuza kwa Watanzania inaendelea kuonekana, ni juzijuzi tu alileta lipstick zenye jina la KISS BY WEMA.

Sasa leo July 11 2016 kupitia Instagram yake Wema Sepetu ametangaza rasmi ujio wa bidhaa yake nyingine ambayo hii ni ya mguuni na iko simple kwa namna hiyo.

Kaandika ‘mara nyingi napenda sana viatu vya chini na vya asilia… nikajionea kwanini nisitengeneze cha aina hiyo?jipatieWema sepetu flops kwa shilingi 12000 kwa jumla na 15000 rejareja, toa oda yako sasa na tutakizindua rasmi tar 29 ambapo mwenyewe ntakuuzia…#UsikuWaWazaramu Loading….. namba ya kupiga kwa ajili ya kuplace order yako ni 0655066565…. vipo design nyiiiingi na rangi nyingi mnoooo’


Idadi ya magari yenye namba binafsi Arusha imetajwa na kufikia magari 6

Serikali ilitangaza kwamba wanaotumia namba binafsi za magari kote Tanzania watatakiwa kulipa shilingi milioni 10 kwa kipindi cha miaka tatu ikiwa ni ada mpya na sio milioni tano kama ilivyokuwa awali.

Wakati ada hiyo mpya ikianza kufanya kazi, meneja wa TRA Arusha April Mbaruku amesema idadi ya magari yenye namba binafsi kwenye mkoa huo ambayo yalilipiwa kipindi cha ada ya milioni tano ni sita tu na hakuna gari lolote lililolipiwa ada mpya ya milioni kumi.



VIDEO: Show ya usiku wa ‘Moyo Mashine’ na Ben Pol

kama ni mpenzi wa burudani na kuparty ‘Usiku wa Moyo mashine’ na mkali wa RnB Ben Pol umefanyika July 10 2016 ndani ya Maisha Basement Dar es salaam, unaweza kiangalia video hii hapa chini..Jinsi ulivofaana na kuwa usiku mwananaaaaa

VIDEO By AyOTv




Uharibifu wa ajali ya Lori daraja la Kigamboni jana matengenezo analipia nani?


Ilitokea ajali ya Lori lililokua na Kontena kwenye daraja la Nyerere Kigamboni Dar es salaam usiku wa kuamkia July 11 2016 ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi pamoja na eneo la barabara kuharibiwa, Meneja msimamizi kwenye hili daraja Gerald Sondo kaongea hapa chini kwenye hii video.akihojia na AyoTv

Mpaka mwaka 2030 kila nyumba Tanzania itakua na umeme



Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amezindua mpango wa nishati endelevu kwa wote (SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030 ambapo amesema uwekezaji wa umeme vijijini awamu ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.

>>>“Mpango huu umelenga kukamilika mwaka 2030 lakini sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na programu hii italifanya taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu apate umeme”

“utasaidia suala la ajira na kutokomeza umaskini, kwahiyo kama nchi tuko katika ngazi za juu za huu mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali” – Profesa Muhongo


‘Programu hii ya umoja wa mataifa itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani inafanana sana na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi kutokana na gesi, makaa ya mawe, umeme wa maporomoko ya maji, umeme wa Jua, joto ardhi na mabaki ya mimea’

Mashirika mengi yamesaidia katika kufanikisha upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo imetoa dola milioni 200, umoja wa ulaya umetoa Euro milioni 180, nchi za Nordic zimetoa dola milioni 300 pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika nayo imetoa fedha.


UEFA wametaja kikosi bora cha michuano ya Euro 2016

Siku moja baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika na timu ya taifa ya Ureno kutwaa taji Kombe hilo, leo July 11 2016 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetaja majina ya wachezaji 11 bora wanaounda kikosi bora cha Euro 2016.

UEFA wametaja majina 11 ya wachezaji kutoka nchi za Ureno, Ufarasa, Ujerumani na Wales, kwa upande wa Ureno wametoa jumla ya wachezaji wanne, Ujerumani watatu, Ufaransa na Wales wawili wawili kila timu, lakini kama utakuwa unakumbuka Ronaldo bado ni mmoja kati ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha muda wote cha Euro

PICHA: Mapokezi ya timu ya taifa ya Ureno baada ya kutua Lisbon na Kombe

Usiku wa July 10 2016 timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro, kwa kuifunga timu ya taifa ya Ufaransa kwa jumla ya goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na na Eder dakika ya 109 katika uwanja wa Stade de France.



Baada ya ushindi huo July 11 2016 kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kiliwasili Lisbon Ureno wakiwa na Kombe lao na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa raia wa nchi hiyo, Ronaldo na wachezaji wenzaji waliwasili Ureno na kutembeza Kombe wakiwa katika basi la wazi.