Friday, August 19, 2016

Masanja asema Orijino Komedi imemalizana na polisi, ni issue ya kuvaa sare za polisi

Baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwakamata baadhi ya wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Masanja Mkandamizaji amedai tayari wameshamalizana na jeshi hilo baada ya kuomba msamaha.
Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa yupo honey moon visiwani Zanzibar, amesema ameamua kutoa taarifa hiyo ili kuwaondoa hofu baadhi ya mashabiki pamoja na ndugu.
“Jamani asanteni kwa maombi na meseji zenu kuulizia juu ya inshu ya polisi, tunamshukuru mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha,” aliandika Masanja facebook.
Aliongeza, “Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini akina Joti, Seki, Maclegan,na Wakuvanga wamepata kautamu kidogo kamahojiano. Na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu,”
Wasanii hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa baada ya kuvaa sare zinazofanana ya za jeshi la polisi katika harusi ya msanii mwenzao Masanja Mkanadamizaji.

Hatuna tatizo na Ruby – Yamoto Band (Video)

Yamoto Band wamesema hawana tatizo na Ruby licha ya kutoonekana kwenye video ya wimbo waliomshirikisha, Su.
Hivi karibuni nilikutana na Maromboso na Aslay ambapo miongoni na mambo mengine, niliwauliza kuhusu kama bado wako vizuri na muimbaji huyo ambaye awali ilisemekana kuwa aliwaletea pozi kuonekana kwenye video yao japo naye aliwatupia lawama kuwa walileta ubabaishaji.
“Kila kitu kiko sawa, hakuna utofauti wowote, sijabahatika kuonana na Ruby tangia tumetoa video,” alisema Aslay wakati akifanya mahojiano na bongo 5 angalia hapa:


Mirror avunjika mguu katika ajali ya gari

Msanii wa muziki, Mirror hivi karibuni amepata ajali mbaya ya gari akiwa anaendesha kutoka katika studio za AM Records pande za Tandale akielekea Ununio.
Katika ajali hiyo, muimbaji huyo amevunjika mguu wa kulia na itachukua miezi mitatu kukaa sawa.
“Mguu umevunjika kabisa, kwa hiyo nimefanyiwa upasuaji na wameunga kabisa mfupa. Nipo hospitali ya private ipo Tegeta, wamenifanyia upasuaji wakawaida, na wameniwekea antena za ndani kwa ndani,” Mirror alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Mpaka jana muimbaji huyo alikuwa bado hajaruhusiwa kuondoka katika hospitali ambayo amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Rwanda ya mfuta kazi kocha wa timu ya taifa McKinstry

Kocha wa timu ya taifa ya Amavubi, Rwanda imemtimua kazi kocha wao Mwingereza Jonathan McKinstry kwa matokeo yasiyo ya kuridhisha.
Taarifa hiyo ilitolewa na wizara ya michezo ya Rwanda imethibitisha kuonyeshwa mlango kwa mkufunzi huyo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo kanali Patrice Rugambwa amesema sababu ya kumfuta kazi kocha huyo ni matokeo yasiyo ya kuridhisha ya timu ya taifa Amavubi.
Rwanda kwa sasa ni ya tatu katika kundi lake kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Gabon mwakani ikiwa na alama 6.
Jonathan McKinstry alipewa mkataba wa kuifundisha Amavubi mwaka jana na ukarefushwa mwaka huu baada ya kuiwezesha kucheza robo fainali ya mashindano ya CHAN ilipoondolewa na DRC.
Timu hiyo kwasasa ipo katika nafasi 121 kwa ubora wa FIFA.

Kidogo ya Diamond yapanda daraja BBC Radio 1Xtra

Diamond Platnumz anachekelea tu sasa hivi kwasababu wimbo wake Kidogo aliowashirikisha mapacha wa P-Square umepanda daraja zaidi kwenye playlist za redio yenye heshima kubwa Uingereza, BBC Radio 1Xtra.
Na ili kujua ukubwa wa hiki kilichotokea ni vyema ukafahamu kuwa ni nyimbo chache sana za Afrika zilizowahi kuingia kwenye playlist ya kituo hicho maarufu kwa burudani UK.
Tuliripoti siku chache zilizopita kuwa wimbo wake huo umeingia rasmi kwenye playlist zake lakini ukawa umewekwa kwenye orodha C. Na sasa wimbo huo umepanda hadi orodha B.
Diamond hajaficha furaha yake kufuatia kupanda daraja kwa wimbo wake huo.
“Dear God i wanna thank you, for everything 🙏…. #KIDOGO on the BBC Radio 1xtra PlayList from C list last week to B list this week…. thanks alot BBC Radio 1xtra and my all UK fans for the Big Support,” ameandika kwenye Instagram.
Iwapo wimbo huo utapanda hadi orodha A, maanake ni kuwa utakuwa kwenye rotation kubwa zaidi kwa siku huku pia akipokea mrabaha mkubwa kutokana na kuchezwa ngoma yake – wenzetu hawachezi ngoma za wasanii bure etii!

Snoop Dogg ampa shavu Nay wa Mitego (Video)

Baadhi ya wana hip hop wanadai kuwa Nay wa Mitego hafanyi hip hop halisi, lakini rapper huyo controversial amepata shavu ambalo hakuna msanii wa hip hop Bongo amewahi kulipata – kupewa shavu na rapper mkongwe, Snoop Dogg.
Asante kwa video ya kuchekesha inayomuonesha babu akicheza na mwanamke mwenye makalio ya haja iliyochanganywa na sauti ya wimbo wa mpya wa Nay wa Mitego, Good Time, sauti yake imesikika kwa followers kibao wa Snoop Dogg.
Haijulikani ameipata wapi video hiyo, lakini Snoop ameipost kwenye akaunti yake ya Instagram yenye followers zaidi ya milioni 11.8.
Ndani ya saa 18, video hiyo imepata views 486k na comments 1850.
Snoop aliandika kwenye video hiyo, “Jump jump jump jump.”
Nay ameirepost na kuandika: Mjomba @snoopdogg ametisha sanaaa nadhani Beat na Michano imemkumbusha mbaliii. OldSkul ndani ya NewSkul..! Inaenda mbaaaliiiiii #GoodTime
Bahati mbaya tu kwa Nay ni kwamba followers wengi wa Snoop hawajui kama ni yeye ndiye mwenye wimbo … laiti kama angemtag!

Burna Boy atangaza kustaafu muziki,Lily Allen amtolea uvivu

Msanii wa miondoko ya Dancehall kutoka nchini Nigeria Burna Boy, usiku wa Jumatano hii, August 17, kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliwashangaza mashabiki wake kwa kutangaza kuwa ataacha muziki baada ya tamasha lake litakalofanyika mjini London October 1.
Burna Boy aliandika ujumbe huu ‘Thinking of quitting music for real after d 1st of October maybe.’ Mashabiki wengi walishangazwa na uamuzi huo wa Burna boy wa kuamua kustaafu kufanya mziki mapema.
Lakini Wapo pia mashabiki wengine waliomkejeli Burna Boy kuwa anatafuta kiki zisizo na mpango ili tu kuipromote show yake hiyo. Burna Boy alionekana kukasirishwa na baadhi ya majibu ya mashabiki zake waliokuwa wakimkejeli.
Vile vile Mwimbaji wa kimataifa kutoka Uingereza Lily Allen amemtolea uvivu Burna Boy kuhusu kolabo yao wanayoitarajia kuitoa. Lily Allen alimtumia ujumbe huu Burna Boy ‘@ burnaboy that’s a shame . I was gonna finish our song next week.
Lily Allen

Burna Boy hakukaa kimya na alimjibu Lily Allen kwa maneno haya ‘u know I ain’t going no where man! They don’t even know the amount of waves coming thru!! Can’t wait!!’ the ‘Yawa Dey’.
Muda mfupi baadaye Burna Boy aliwapunguza kidogo presha mashabiki zake kuhusu mustakabali wake wa kustaafu kwa mfululizo wa tweets wenye ujumbe huu
‘I wud quit if it was just me
but I got bruddas that’s Died for this
n I got pple who took their undying
love for me n my music to d grave.’
‘My 1/10/16 concert in London wud b
a great way to say goodbye tho. On d
contrary it will only b d beginning of
new levels unlocked! # Powers’





Bolt achukua dhahabu ya pili mbio za mita 200 Olimpiki Rio

Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt ameshinda mbio za mita 200 katika michuano ya Olympics huko Rio nchini Brazil na kujinyakulia medali ya dhahabu ya pili baada ya kunyakua ya michuano ya mbio za mita 100.
Ameshinda kwa kirahisi mbio hizo za mita 200 kwa kutumia sekunde 19.79. Bolt kwa sasa anahitaji kushinda mbio za mita 4x 100 za kupokezana vijiti ili kukamilisha medali ya tatu ya dhahabu kama alivyofanya katika michuano iliyopita.
Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na kunyakuwa medali ya dhahabu.
Katika matokeo mengine Marekani imenyakulia medali nyingine nne za dhahabu ikiwemo ya mwanariadha wake Ashton Eaton.
Source: BBC

Kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi yafungwa, watoto 37 wafanyiwa upasuaji

Kambi tiba ya upasuaji wa watoto mwenye vichwa vikubwa na mgongo wazi iliyokuwa imeingia katika msimu wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji.
Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto)
Aidha, watoto zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji.
Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.
Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.
Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.
Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena Iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.
Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

Ukimya wa collabo ya Shilole na msanii wa Nigeria, majibu yako hapa….

Najua nina watu wangu ambao watakuwa na maswali mengi juu ya ile ya collabo ya Shilole na staa kutokea Nigeria, Selebobo sasa basi millardayo.com imempata Shilole na kufafanua zaidi juu ya ukimya wa collabo hiyo.
Collabo yangu mimi na Selebobo wimbo upo tayari sema tu kilichobaki ni upande wa video kwahiyo nilikuwa namuuliza kuhusu mapendekezo yake ya location tutakapofanyia hiyo video mpya akapendekeza Nigeria itakuwa ndio location kwahiyo nasubiri tu nikimaliza tamasha la Fiesta nitaenda Nigeria kwaajili ya maandalizi ya video hiyo mpya’-
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Shilole akiongea collabo hiyo @ayo_tv

VIDEO: Ziara ya kushtukiza aliyoifanya DC Ally Hapi katika hospitali ya Mwananyamala

August 18 2016 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Dar es salaam Ally Hapi alifanya ziara katika hospitali ya Mwananyamala na kubaini mapungufu mbalimbali katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa fedha za wagonjwa ambapo inadaiwa hospitali hiyo imekuwa ikitozapesa ya kujiandikisha Shilingi elfu kumi badala ya elfu sita iliyoidhinishwa na Serikali.
DC Hapi amesema…>>>’Nimekuja kuangalia utozaji wa gharama za kadi kwa wagonjwa, nilipewa taarifa kwamba wagonjwa wamepandishiwa bei kutoka shilingi elfu sita hadi elfu kumi jambo ambalo linawafanya masikini kukosa huduma
Nilitoa maelekezo jana lakini bado wanaendelea kutoza elfu kumi, pia utaratibu wa kupandisha hizo fedha haukufuatwa na inaonekana inagusa hadi kwenye gharama za vipimo‘ –Ally Hapi
Nimeagiza fedha ishushwe ibaki vilie ilivyokuwa awali na pili Mkurugenzi na timu yake wachukue hatua kuhakikisha kila mmoja aliyehusika achukuliwe hatua stahiki akiwemo mganga mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala‘ –Ally Hapi

VIDEO: Majibu ya Wenger kuhusu matumizi ya pesa nyingi katika usajili

Najua na watu wangu wa nguvu ambao ni mashabiki wa Arsenal na wanatamani kumuona kocha wao Arsene Wenger akifanya usajili au akitumia pesa nyingi kufanya usajili kama ilivyo kwa Man United na vilabu vingine, ukimuuliza suala la kutumia fedha katika usajili Wenger atakujibu hivi.
“Tumeshuhudia moja kati ya vilabu vya Ligi Kuu England kikimsajili kiungo wa kati kwa fedha nyingi zaidi, kitu ambacho sisi hatujafanya ni muhimu kutumia pesa katika usajili lakini ni muhimu sana kutumia pesa kwa usahihi yaani kwa utaratibu mzuri”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Wenger sio kocha mwenye tamaduni za kusajili wachezaji kwa dau kubwa kama walivyofanya Man United kwa Paul Pogba kumsajili kwa pound zaidi ya milioni 100 akitokea Juventus ya Italia, hivyo kwa sasa yupo katika shinikizo la mashabiki na waandishi ambao wamekuwa wakikosoa ubahili wake.

Habari 5 ‘HOT’ kwenye TV za Tanzania August 18 2016

Habari zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 18 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano ‘Hot‘ kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka ITV
Wakadiriaji majenzi watakiwa kuepuka rushwa na kulinda taaluma yao.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (Mhe.Prof.Makame Mbarawa) amewaeleza wakadiriaji hao kuwa na mkadiriaji yeyote atakae kosa uwadilifu serikali itamfutia usajili na kuongeza kuwa ni bora kuwa na wataalamu wachache watakaofanya kazi na walio waadilifu pia kuwa na viwango vya kimataifa.
Habari kutoka Azam TV
Udhibiti dhidi ya matumizi ya Tumbako bado.
Waziri wa afya (Mhe.Ummy Mwalimu) amesema haya kuhusu utumiaji wa Tumbaku unaoendelea nchini akiongelea mkakati wa serikali kupunguza matumizi ya Tumbaku kufikia asilimia 25 mpaka mwaka 2030
>>>’ Tukiongeza kodi za bidhaa za Tumbaku kwa asilimia 10 kwa miaka mitano, kwanza tutaongeza mapato ya serikali kwa asilimia 39.9 mpaka  47.5 lakini pia tutaokoa vifo vya watanzania takriban elfu 63 kwahiyo kodi ndiyo moja wapo ya njia bora na sahihi za kudhibiti matumizi ya Tumbaku nchini‘- Waziri wa afya (Mhe.Ummy Mwalimu)
Habari kutoka Star TV
Mgogoro wa Ardhi
>>>‘Haiwezi kuwa na haitatokea chini ya awamu ya tano kwamba mtu mgeni atapita kila mahali kwenye kona ya nchi hii atakusanyakusanya ardhi alafu atachukua hati , nchi hii haiwezi toa hati kwa namna hiyo‘- Waziri William Lukuvi
Habari kutoka Azam TV
Rais Magufuli amekutana na katibu Mkuu wa EAC Ikulu Dar es salaam
>>>’Nimemweleze Rais kwamba tuna project nyingi sana na inahusiana vizuri na vipaumbele vyetu,na tenatunangalia jinsi tunaweza kufanya kazi na wananchi wa Eact Africa wapate faida‘- Katibu Mkuu wa EAC ( Liberat Mfumukeko) 
Habari kutoka TBC
Amani Tanzania, viongozi wakubwa wa dini nchini wameongelea juu ya swala hili
>>>’Ni vizuri basi watanzania hii tarehe moja tuwe na tahadhari nayo endapo serikali itajipanga kupokea maandamano hayo na kuyaruhusu watanzania waandamane, lakini kama serikali itabaki na msimamo wake kuwaingiza watanzania barabarani  wakaja kupata ulemavu na kuumia na pengine vifo vikatokea si jambo la busara‘  – Mwenyekiti kamati ya Amani Dar es salaam (Sheikh Alhad Musa Salum)

KRC Genk imelazimishwa sare na Lokomotiva ugenini, Samatta akipachika goli

Usiku wa August 18 2016 michezo ya Play offs ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Europa League ilichezwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, moja kati ya michezo ya Europa iliyochezwa usiku wa August 18 ni mchezo kati yaLokomotiva Zagreb ya Croatia dhidi ya KRC Genk inayochezewa na Mbwana Samatta.
Katika mchezo huo uliyochezwa Croatia yaani katika uwanja wa nyumbani waLokomotiva, umemalizika kwa sare ya goli 2-2, Genk inayochezewa na mtanzaniaMbwana Samatta ilianza kupata goli la kwanza kwa mkwaju wa penati kupitia mjamaicaLeon Bailey dakika ya 47 na baadae Mbwana Samatta dakika ya 52.
Licha ya kuwa Lokomotiva walikuwa nyumbani na kufanikiwa kusawazisha goli zote mbili kupitia kwa Mirko Maric dakika ya 51 na Ivan Fiolic dakika ya 59, KRC Genk ilitawala mpira kwa asilimia 60 na kuwaacha wenyeji wao wakimiliki mpira kwa asilimia 40, Kwa matokeo hayo Genk itahitaji suluhu au sare ya goli 1-1 katika mchezo wa marudiano August 25 katika uwanja wao nyumbani.