Tuesday, July 12, 2016

Azam Tv Kuonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara, kumwaga Sh 23 bilioni Ligi Kuu


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF leo July 12 2016 limetangaza good news kwa mashabiki wa soka ambao huenda huwa wanakosa muda wa kwenda uwanjani kuangalia mechi, TFF leo imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano na Azam TV kwa ajili ya kuendelea kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.

Mkataba huu wa Azam TV sasa klabu itakuwa inapewa milioni 126 kwa awamu tatu tofauti na awali ilivyokuwa milioni 100, awamu ya kwanza na pili zitatolewa milioni 42, halafu awamu ya mwisho klabu inayomaliza nafasi za juu zaidi inalipwa zaidi kuliko iliyopo nafasi ya chini, hii inatokana na TFF na Azam TV kuamua kuleta ushindani.

Hafla ya kuongeza udhamini huo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na katibu mkuu Selestine Mwesigwa huku kampuni ya Azam ikiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wake Tido Mhando

Kwa mujibu wa mtandao wa instagram wa Azam umetoa taarifa hii:


Azam Media Ltd yashinda Tenda ya Kuonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine tena, udhamini mnono na wa Kihistoria Bilioni 23

No comments:

Post a Comment