Tuesday, July 12, 2016

Umefichuka mpango wa Arsenal ili kumpata Gonzalo Higuan



Alfajiri ya July 12 2016 ikiwa ni siku moja imepita toka michuano ya Euro 2016 imalizike, vilabu mbalimbali vya soka barani Ulaya vimerudi kwa kasi katika mbio za kuwania wachezaji nyota ili waboreshe vikosi vyao, Arsenal imeripotiwa na mtandao wa Di Marzio kurudi tena katika mbio za kumuwania mshambuliaji Gonzalo Higuan.


Higuan

July 12 Arsenal imetajwa kuwa katika mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya Napoli ya Italia, uhamisho wa Higuan kujiunga na Arsenal unaripotiwa kuwa tofauti, kutokana na Arsenal kutokuwa tayari kutoa Euro milioni 50 zinazohitaji na  Napoli kama dau la usajili. 

 Giroud

Arsenal wanataka kumsajili Higuan kwa dau pungufu la Euro milioni 50, pamoja na kumtoa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ufaransa Oliver Giroud kwenda Napoli kama sehemu ya kukamilisha usajili wa Gonzalo Higuan kujiunga na Arsenal, ambaye anahusishwa kuwa katika mipango ya Wenger kwa mara nyingine tena

No comments:

Post a Comment