July 12 2016 Kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea
hii hekaheka kutokea Tandale Hospitali Dar es salaam ambapo mgonjwa
aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje
usiku kucha, mashuhuda wanasema hospitali walipopewa taarifa hawakujali.
Mashuhuda
wanadai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000
ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye HekaHeka ya leo.
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa……….>>>’kaja
toka jana kaingia ndani baada ya kuingia ndani kwa kuwa alikuwa
hajiwezi alivyotoka akafikia akakaa hapa, basi alipofikia akalala mpaka
leo asubuhi, tukawa waoga, tukaenda kituo cha polisi tukatoa taarifa,
akaja polisi akamwangalia nae akaondoka, mwenyekiti akarudi tena nae
akaondoka, mpaka inafikika saa 6;30 akawa anang’ata ulimi anakufa’
Kuisikiliza full story, bonyeza link hapa chini
No comments:
Post a Comment