Taarifa hiyo ilitolewa na wizara ya michezo ya Rwanda imethibitisha kuonyeshwa mlango kwa mkufunzi huyo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo kanali Patrice Rugambwa amesema sababu ya kumfuta kazi kocha huyo ni matokeo yasiyo ya kuridhisha ya timu ya taifa Amavubi.
Rwanda kwa sasa ni ya tatu katika kundi lake kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Gabon mwakani ikiwa na alama 6.
Jonathan McKinstry alipewa mkataba wa kuifundisha Amavubi mwaka jana na ukarefushwa mwaka huu baada ya kuiwezesha kucheza robo fainali ya mashindano ya CHAN ilipoondolewa na DRC.
Timu hiyo kwasasa ipo katika nafasi 121 kwa ubora wa FIFA.
No comments:
Post a Comment