Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto)
Aidha, watoto zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji.
Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.
Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.
Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.
Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena Iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.
Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.
No comments:
Post a Comment