Kile kilichodhamiriwa kuwa ni utani kuhusu Usain Bolt, kimegeuka kuwa kitimoto kwa mtangazaji maarufu wa TV nchini Marekani, Ellen DeGeneres.
Jumatatu hii mtangazaji huyo wa talk show alitumia Twitter kuweka picha iliyotengenezwa na kumuonesha akiwa amebebwa mgongoni mwa mshindi huyo wa medali ya dhahabu raia wa Jamaica.
Picha hiyo ni ile ambayo sasa imekuwa maarufu sana mtandaoni ikimuonesha Bolt akichekelea ukingoni mwa mbio za mita 100 kwenye mashindano ya Olympics mjini Rio.
Maneno kwenye tweet hiyo yalisomeka: This is how I’m running errands from now on.”
Tofauti na matarajio ya Ellen, baadhi ya watumiaji wa Twitter waliitafsiri picha hiyo kama ishara ya kibaguzi kwa mzungu amebebwa mgongoni na mtu mweusi.
Lakini wengine walimtetea DeGeneres kuwa yeye na Bolt, aliyewahi kuhojiwa kwenye kipindi chake ni marafiki wakubwa. Mmoja aliandika: “If Usain was white, y’all wouldn’t care. We all know Ellen isn’t racist & didn’t mean any harm by that. Stop it.”
Ellen alijibu baadaye: I am highly aware of the racism that exists in our country. It is the furthest thing from who I am.”
No comments:
Post a Comment