Thursday, August 18, 2016

Mwandishi wa ‘Work’ ya Rihanna alitaka kumpa wimbo huo Alicia Keys

Mara nyingi muziki wa Marekani umekuwa ukiandikwa nyuma ya pazia na waandishi ambao wengi wao hawajulikani sana kwa watu kama wasanii wenyewe. Na wakati mwingine mwandishi huandika wimbo akimlenga msanii fulani lakini ukaja kuimbwa na msanii mwingine kabisa.
Na sasa mwandishi wa hit ya Rihanna na Drake, Work, PARTYNEXTDOOR amedai kuwa awali aliuandika wimbo huo kwa lengo la kumpa Rihanna, lakini label yake haikuupenda na hivyo alifikiria kumpa Alicia Keys.
“Label yake [Rihanna] haikuwa inajali kuhusu muziki wa Caribbean wakati huo,” aliliambia The New York Times na kuongeza kuwa kidogo aamue tu kukaa nayo kabla ya kufikiria kumpa Alicia Keys. Mwisho wa siku alisema Rihanna aliupigania.
PARTYNEXTDOOR anadai Rihanna alimwambia kuwa Work ni wimbo unaopendwa zaidi na familia yake.
Work ni wimbo uliofanywa vizuri kwenye chati duniani ikiwa ni pamoja na kukaa kwenye chati ya Billboard kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment