
Waziri wa
nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amezindua mpango wa nishati
endelevu kwa wote (SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa
nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030 ambapo amesema uwekezaji wa umeme
vijijini awamu ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.
>>>“Mpango
huu umelenga kukamilika mwaka 2030 lakini sisi Tanzania kabla ya mwaka
huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na programu hii italifanya
taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu
apate umeme”
“utasaidia suala la ajira na
kutokomeza umaskini, kwahiyo kama nchi tuko katika ngazi za juu za huu
mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali” –
Profesa Muhongo
‘Programu hii ya umoja wa mataifa
itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani
inafanana sana na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi
kutokana na gesi, makaa ya mawe, umeme wa maporomoko ya maji, umeme wa
Jua, joto ardhi na mabaki ya mimea’
Mashirika mengi yamesaidia katika
kufanikisha upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo
imetoa dola milioni 200, umoja wa ulaya umetoa Euro milioni 180, nchi za
Nordic zimetoa dola milioni 300 pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika
nayo imetoa fedha.
No comments:
Post a Comment